TUNAPENDA KUSHIRIKIANA NAWE KATIKA
UNDISHI WA KATIBA YA USHIRIKA WA VIJANA WA KIKRISTO TANZANIA.
- WAPENDWA TUNAOMBA MPITIE RASIMU HII YA KATIBA
ILIYOTUMWA KWA WACHUNGAJI KISHA KOSOA,TOA MAONI,ONGEZA KITU AU SHAURI
JAMBO AU ULIZA. KISHA TUMA KWENYE EMAIL HII jesus4youth@gmail.com
RASIMU YA KATIBA YA USHIRIKA WA VIJANA WA KIKRISTO TANZANIA
1. SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
Ibala 1.
JINA LA KIKUNDI.Kikundi hiki kitajulkana kama CHRISTIAN YOUTH FELLOWSHIP IN
TANZANIA (CYFT) kwa kiswahili USHIRIKA WA VIJANA WA KIKRISTO TANZANIA
S .L.P.
245, Mbeya.
Mahali
Tulipo MBEYA.
Dira.
Dira
ya Ushirika wa vijana wa kikristo Tanzania “Ni kuunganisha vijana wa
kikristo Tanzania kuhakikisha wanamtumikia Mungu kwa pamoja bila kujari
udhehebu wao.”kwa kutambua umuhimu wa kumtumikia Mungu tukiwa bado vijana na
kuondoa mipaka ya madhehebu tukana ni vema tukaungana ili kuujenga Mwili wa
Kristo katika maeneo yetu tunayo ishi,fanya kazi, soma na Kuabudu. Hivyo
tukaona vema kuanzisha Ushirika wa Vijana Wa Kikristo Tanzania kwa ngazi ya Taifa,
Mikoa na Wilaya.
Dhima
Ni kuunganisha vijana wa kikristo TANZANIA ili tumtumikie MUNGU.Lengo ni
kuhubiri neno la Mungu katika kila eneo kwa njia zote yaani
Uimbaji,uinjilisti,uwalimu,unabii,uchungaji na utume.kuandaa mikutano ya
injili,semina za ndani na nje,makongamano ya kusifu,kuabudu na maombi.
Kutembeleana,kushauriana,kusaidiana,kubadilishana mawazo,ujuzi na ufahamu
kuhusu maisha ya vijana ili kufanikiwa kiroho na mwili.Kusaidiana katika
changamoto za ujana,Hasa katika uchumi,Mahusiano,Ndoa,Huduma,Elimu,jamii na
kazi za kila siku
SEHEMU YA PILI.
Ibala 2. IMANI
a)
Tukiwa kama Ushirika Wa Vijana wa
Kikristo Tanzania tunamkubari YESU KRITO kuwa ni BWANA na MWOKOZI wa watu wote.
b)
Tunayaamini maandiko matakatifu
yaani BIBLIA kuwa ni NENO la Mungu nalo ni kweli na takatifu.
c)
Tunaamini kuwa YESU KRISTO alikufa
na akafufuka na kuwa ROHO MTAKATIFU anafanya kazi kati yetu na MUNGU baba ndiye
muumba wa mbingu na nchi.
d)
Hatu amini katika Dhehebu,dini au
Mtu binafsi.
SEHEMU YA TATU
Ibala 3:MADHUMUNI YA USHIRIKA.
1.Kuhubiri
injili ili watu wampokee YESU KRISTO kuwa BWANA naMWOKOZI wa maisha yao na
kwasaidia vijana waishi kwa kufuata Misingi ya Kristo huku wakishuhudia na
kutangaza/kuhubiri habari njema na kumtumikia MUNGU katika nchi yao na
ulimwengu wote.
2.Madhumuni
Mahususii
(i)
Kuandaa semina,kambi za maombi na
mikesha ya kusifu na kuabudu kwa ajili ya Taifa la Tanzania.
(ii)
Kuhamasisha vijana wa kikristo bila
kujali udhehebu wao kumtumikia Mungu katika maeneo yao na Tanzania kwa
ujumla.
(iii)
Kufungua miradi itakayo endeshwa na ushirika
wa vjana wa kikristo Tanzania.
(iv)
Katafuta na kutoa fulsa za ajira kwa
vijana bila kujali dhehebu dini au kabila
(v)
Kutembeleana,kushauriana,kusaidiana,kubadilishana
mawazo,ujuzi na ufahamu kuhusu maisha ya vijana ili kufanikiwa kiroho na
mwili.Kusaidiana katika changamoto za ujana,Hasa katika
uchumi,Mahusiano,Ndoa,Huduma,Elimu,jamii na kazi za kila siku.
SEHEMU YA NNE
Ibala4:UANACHAMA NA MASHARITI.
Kijana
kutoka katika kanisa lolote Tanzania linalotambulika kiserikali na kijami
(i)
Jinsi ya
kujiunga na Umoja.
a)
Atajaza fomu ya maombi ya uwana
chama wa kudumu kwa Tawi,Wiaya na Mkoa Husika itakayo patikana Katika ofisi na
tovuti/blog au mwakilishi wa umoja huu.
b)
Atajadiliwa na kukubaliwa na
wanachama wa ngazi husika
c)
Atapewa taarifa za kuwa Mwanachama
na Viongozi wa ngazi husika.
(ii)
Mashariti
ya Uwana chama.
(i)
Atakubaliana na katiba ya Ushirika
Wa Vijana Wa Kikristo Tanzania (UVIKITA)
(ii)
Baada ya kujiunga atatakiwa kulipia
ada kitambulisho cha mwanachama kila mwaka kwa ngazi husika.
(iii)
Atashiriki katika shughuli za umoja
na kutoa michango Muhimu pale inapotakiwa
(iv)
Awe ni mtanzania mwenye akili timamu
na mwenye umri usio pungua miaka 18
(v)
Awe mwaminifu kwa Mungu na mwenye
utayari wa kufanya kazi ya Mungu.
Ibala5: HAKI ZA MWANACHAMA
(i)
Mshirika atakuwa na haki sawa katika
umoja bila kujali jinsia yake.
(ii)
Anayo haki ya kuchangia mawazo na ya
kupata taarifa mbalimbali zinazomuhusu umoja
(iii)
Kila mwanachama anayo haki ya
kutumia kipaji chake kubuni, kuunda na kutengeneza kitu chochote anacho fikiria
kwa kuwashirikisha na kukubaliana na viongozi wa umoja.
(iv)
Mwana chma ana haki ya kukosoa au
kukosolewa au kutoa maoni ya kuimarisha umoja
(v)
Ana haki ya kushitaki/kushitakiwa kwenye
vyombo vya sheria
(vi)
Haki ya kuajiriwa na Ushirika huu na
afuate mkataba wa kazi apewe muda na ausome na kuridhia.
Ibala6: KUKOMA AU MWISHO WA
MWANACHAMA
(i)
Mwanachama atapoteza uwana chama
endapo atakiuka Katiba ya UVIKITA
(ii)
Kutopoteza ushuhuda mzuri wa
Kikristo kwa umoja huu na jamii inayo mzunguka
(iii)
Kukiuka,kuupuuza au kufanya jambo
lililo nje na lengo au makubalino ya umoja kwa manufaa bainafsi.
SEHEMU YA TANO
UONGOZI
Ibala 7:Viongozi
Muundo
wa ungozi katika Ushirika huu unanzia ngazi ya Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.
a)
Muundo wa ungozi kwa ngazi ya Tawi,
Wilaya na Mkoa utakuwa:-
(i)
Mwenyekiti
(ii)
Makamo mwenyekiti
(iii)
Katibu
(iv)
Makamo katibu
(v)
Mhazini
(vi)
Mwenyekiti wa Maombi
b)
Muundo wa uongozi kwa ngazi ya Taifa
utakuwa:-
(i)
Mratibu mkuu
(ii)
Katibu mkuu
(iii)
Mhazini
(iv)
Mwenyekiti wa Maombi
(v)
Makamo mwenykiti wa maombi
Ibala8: SIFA ZA VIONGOZI
Viongozi
wa ushirika huu wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:-
a)
Awe mwaminifu kwa Mungu.
b)
Awe anafuata katiba ya ushirika.
c)
Awe mwenye kujituma,
kujitolea, mpenda kazi na mwenye ushirikiano na wengine bila kujali jinsia
d)
Awe mwaminifu na muwazi kwa wengine.
e)
Awe mwenye unyenyekevu (utii) asiye
tanguliza maslahi binafsi
f)
Awe anayetoka kwenye kanisa la
kikristo linalo tambulika kiserikali na kijamii na lenye ushuhuda mzuri.
g)
Awe anatambulika kwa uongozi wa
Kanisa lake na mwenye kushirikiana vema.
Ibala 9: WAJIBU WAVIONGOZI
KITAIFA, MKOA, WILAYA NA TAWI
1)
Mratibu kuu,Mwenyekiti wa Tawi,
Wilaya, Mkoa.
(i)
Kusimamia na kuaratibu shughuli zote
ushirika kwa ngazi husika
(ii)
Kuitisha vikao vya kamati kuu kwa
kupitia katibu.
(iii)
Mwendeshaji na msimamizi wa matukio
yote kwa ngazi husika
(iv)
Mshauri katika shughuli za Mikoa
(Mratibu mkuu Taifa)
(v)
Kuhusika katika maswala yote fendha
kwa kutia sahihi
(vi)
Kubeba dhamana ya mali zote za
ushirika.
2)
Katibu wa Taifa, Mkoa, Wilaya na
Tawi
(i)
Ndiye mtendaji mkuu na mfuatiliaji
wa shughuli zote kwa ngazi husika
(ii)
Kukusanya na kutunza taarifa na
takwimu zotekitaifa
(iii)
Kupanga na kutoa taaria za matukio
ya kitaifa ikiwa na vikao.
(iv)
Mwandishi wa vikao vyote vya ushuka
na kusoma makubaliano.
(v)
Kutuma na kupoke barua zote na
kuzifikisha mahali husika
(vi)
Kubeba dhamana ya mali zote za
ushirika
3)
Mtunza Hazina
(i)
Kupokea na kutoa fedha kwa shughuli
zote za ushirika
(ii)
Kutunza mali na kusimamia miradi
yote ya ushirika(kubeba dhamana)
(iii)
Kupeleka fedha Benki na kutunza
kumbukumbu za kifadha kwa ushirila
(iv)
Kutoa stakabadhi kwa kila fedha ya
malipo na kutunza vitabu vya risiti
(v)
Kutia sahihi Benki wakati wa kuweka
au kutoa fedha
4)
Mwenyekiti wa Maombi
(i)
Kundaa shughuli zote za kiroho na
maombi kwa ngazi husika
(ii)
Kuhakikisha injili neon la Mungu
linafika maeneo yote
(iii)
Kulea na kusimamia maisha ya kiroho
ya kanisa kwa ngazi husika
(iv)
Kushiriki katika matukio ya umoja
kwa ngazi husika
(v)
Kubeba dhamana ya mali zote za
ushirika kwa ngazi husika.
SEHEMU YA SITA
MUUNDO
Ibala10:Kamati kuu ya Tawi
(i)
Kamati kuu
ya tawi inahushisha:-
Mwenyekiti. Makamu mwenykiti.
Katibu. Mtunza hazina. Mwenykiti wa maombi. Makamu mwenyekiti wa maombi na mshauri
wa tawi.
(ii) Wajibu wa kamati hii utakuwa:
a)
Kusimamia shughuli zote za tawi.
b)
Kuandaa agenda na kusimamia vikao
vya tawi
c)
Kuandaa na kutoa taarifa zinazohusu
shughuli zote za uendeshaji wa tawi kwa halmashauri kuu ya tawi na kamati kuu
ya wilaya.
d)
Kuaandaa vikao visivyopungua vinne
kwa mwaka kama kamati kuu.
e)
Kuandaa mikutano ya halmashauri kuu
ya tawi isiyo pungua mitatu kwa mwaka.
f)
Kushiriki na kuhusika kwenye matukio
ya wilaya,mkoa na Taifa kwa ujumla
g)
Kuandaa na kufanya matukio kwa
wilaya yao.
h)
Kuhudhuria na kushiriki vikao vya
halmashauri kuu ya wilaya yao
i)
Kujadili
mwenendo mzima wa umoja na kupanga mikakati ya kuiendesha.
j)
Kupanga bajeti ya umoja na kuiwasilisha kwenye
Halmashauri kuu.
k)
Kuibua
na kupanga miradi mbalimbali ya umoja na kuijadili kwenye halmashauri kuu.
l)
Kupanga
mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya umoja
m)
Kupitia maombi ya wanachama na kuyajibu na
baadaye kuyawasilisha kwenye halmashauri kuu
Ibala 11:Kamati kuu ya Wilaya
(i)
Kamat kuui
ya wilaya inahusisha:-
Mwenyekiti. Makamu mwenykiti.
Katibu. Mtunza hazina. Mwenykiti wa maombi. Makamu mwenyekiti wa maombi na mshauri
wa wilaya
(ii)
Wajibu wa
kamati hii utakuwa:-
a)
Kusimamia shughuli zote za wilaya.
b)
Kuandaa agenda na kusimamia vikao
vya wilaya
c)
Kuandaa na kutoa taarifa zinazohusu
shughuli zote za uendeshaji wa wilaya kwa halmashauri kuu ya wilaya na kamati
kuu ya mkoa.
d)
Kuaandaa vikao visivyopungua vinne
kwa mwaka kama kamati kuu.
e)
Kuandaa mikutano ya halmashauri kuu
ya wilaya isiyo pungua miwili kwa mwaka.
f)
Kufanya ziara za mara kwa mara
katika matawi yao
g)
Kushiriki na kuhusika kwenye matukio
ya mkoa na Taifa kwa ujumla
h)
Kuhudhuria na kushiriki vikao vya
halmashauri kuu ya Mkoa wao.
i)
Kujadili mwenendo mzima wa umoja na kupanga
mikakati ya kuiendesha.
j)
Kupanga bajeti ya umoja na kuiwasilisha kwenye
Halmashauri kuu.
k)
Kuibua
na kupanga miradi mbalimbali ya umoja na kuijadili kwenye halmashauri kuu.
l)
Kupanga
mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya umoja
m)
Kupitia maombi ya wanachama na kuyajibu na
baadaye kuyawasilisha kwenye halmashauri kuu
Ibala12 :Kamati ya mkoa.
(i)
Kamati kuu
ya mkoa inahusisha:-
Mwenyekiti. Makamu mwenykiti.
Katibu. Mtunza hazina. Mwenykiti wa maombi. Makamu mwenyekiti wa maombi na
mshauri wa mkoa.
(ii)
Wajibu wa
kamati hii utakuwa:-
a)
Kusimamia shughuli zote za wilaya,mkoa
na Taifa.
b)
Kuandaa agenda na kusimamia vikao
vyote vya mkoa
c)
Kuandaa na kutoa taarifa zinazohusu
shughuli zote za uendeshaji wa mkoa kwa halmashauri kuu ya mkoa na kamati kuu
ya Taifa.
d)
Kuaandaa vikao visivyopungua sita
kwa mwaka kama kamati kuu.
e)
Kuandaa mikutano ya halmashauri kuu
ya mkoa isiyo pungua miwili kwa mwaka.
f)
Kufanya ziara za mara kwa mara
katika matawi na wilaya zao
g)
Kushiriki na kuhusika kwenye matukio
ya mkoa na Taifa kwa ujumla
h)
Kuhudhuria na kushiriki vikao vya
halmashauri kuu ya Mkoa na Taifa.
i)
Kujadili mwenendo mzima wa umoja na kupanga
mikakati ya kuiendesha.
j)
Kupanga bajeti ya umoja na kuiwasilisha kwenye
Halmashauri kuu.
k)
Kuibua
na kupanga miradi mbalimbali ya umoja na kuijadili kwenye halmashauri kuu.
l)
Kupanga
mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya umoja
m)
Kupitia maombi ya wanachama na kuyajibu na
baadaye kuyawasilisha kwenye halmashauri kuu
Ibala13 :Kamati kuu ya Taifa
(i)
Kamati kuu
ya taifa inahusisha:-
Mratibu mkuu. Katibu mkuu. Mtunza
hazina. Mwenykiti wa maombi. Makamu mwenyekiti wa maombi na mshauri wa Taifa.
(ii)
Wajibu wa
kamati hii utakuwa:-
a)
Kusimamia shughuli zote za Taifa.
b)
Kuandaa agenda na kusimamia vikao
vyote vya Taifa
c)
Kuandaa na kutoa taarifa zinazohusu
shughuli zote za uendeshaji wa Taifa kwa halmashauri kuu ya Taifa.
d)
Kuaandaa vikao visivyopungua viwili
kwa mwaka kama kamati kuu.
e)
Kuandaa mkutano wa halmashauri kuu
ya Taifa kwa mwaka.
f)
Kufanya ziara za mara kwa mara mikoani na wilaya inapobidi.
g)
Kushiriki na kuhusika kwenye matukio
ya mikoa na Taifa.
h)
Kuhudhuria na kushiriki vikao vya
halmashauri kuu ya Taifa na mikoa.
i)
Kujadili mwenendo mzima wa umoja na kupanga
mikakati ya kuiendesha.
j)
Kupanga bajeti ya umoja na kuiwasilisha kwenye
Halmashauri kuu.
k)
Kuibua
na kupanga miradi mbalimbali ya umoja na kuijadili kwenye halmashauri kuu.
l)
Kupanga
mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya umoja
m)
Kupitia maombi ya wanachama na kuyajibu na
baadaye kuyawasilisha kwenye halmashauri kuu
Ibala 14:Halmashauri kuu.
(i)
Halmashauri
kuu inahusisha:-
Wajumbe wote wa umoja toka matawini
(viongozi) na wawakilishi wawili walio teuliwa na wachama wa ushirika kwa ngazi ya wilaya mkoa
na Taifa.Na wanachama wote wa ushirika kwa ngazi ya Tawi.Washauri wakiwa ni
wajumbe waalikwa.
(ii)
Wajibu wa halmashauri kuu.
a)
Mkutano Mkuu ndiyo kikao chenye madaraka ya juu
ya uamuzi wa mwisho katika umoja
b)
Kupokea
taarifa za umoja kwa ngazi husika na
kuzipitisha au kuzijadili
c)
Kuchagua viongozi wakuu wa umoja kwa ngazi
husika.
d)
Kujadili mambo mbalimbali ya kuweza kuboresha
umoja
e)
Kufanyia
marekebisho katiba ya umoja kama ikibidi ili kuendana na mahitaji ya wakati
f)
Kupitisha bajeti na majina ya wanachama wapya
SEHEMU YA SABA
UCHAGUZI:
Ibala 15:Muda wa Uchaguzi.
(i)
Uchaguzi wa viongozi kwa ngazi zote
utafanyika kila baada ya miaka miwili.
a)
Uchaguzi wa ngazi ya tawi utafanyika
mwezi Februari na ngazi ya wilaya mwezi april
b)
Uchaguzi ngazi ya mkoa utafanika
mwezi wa Juni na kwa ngazi ya Taifa utafanyika mwezi Disemba
c)
Watakao chaguliwa ni vijana wa
kikristo wanaotoka katika madhebu ya kikristo na yanayotambulika kisheria na
kijamii yenye ushuhuda mzuri na kukubarika.
.
(ii)
Muda wa kuongoza ni miaka miwili,
kiongozi anaweza kuchaguliwa tena endapo atafanya kazi vema
Ibala 16:Kutambulisha Wagombea
(i)
Wagombea kwa ngazi ya tawi/wilaya
watatambulishwa mara moja kabla ya uchaguzi
(ii)
Wagombea kwa ngazi ya mkoa na Taifa
watatambulishwa mara tatu kwa wajumbe wa Halmashauri kuu kabla ya uchaguzi.
Ibala 17:Upigaji Kura.
(i)
Uchaguzi utakuwa ni wa siri
(ii)
Yatapendekezwa majina matatu (3) kwa
kila kiti na kuungwa mkona za zaidi ya nusu ya wajumbe wa halmashauri kuu
(iii)
Atakayepata kura zaidi ya nusu
atakuwa kiongozi
(iv)
Ikitokea kufungana kwa kura
watarudia uchaguzi mara tatu na msimamizi atakuwa na kura ya uwamuzi
(v)
Mwanachama asie kuwa kijana wa
kikristo, washauri na wachungaji hawatapiga kura.
Ibala 18:Viongozi waliochaguliwa.
(i)
Viongozi wapya waliochaguliwa watatangazwa
na msimamizi wa uchaguzi kwa kusimamishwa na kutambulishwa mbele ya halmashauri
kuu
(ii)
Watakabidhiwa uongozi na kimbukumbu
za umoja na kusimikwa ndani ya siku tatu.
(iii)
Viongozi hawa watasimikwa na
wachungaji/mchungaji atakaye alikwa kwaajili shughuli hii.
Ibala 19: MAPATO NA MATUMIZI.
a)
Mapato.
Ushirika utajipatia mapato kwa
shughuli zilizo anzishwa na umoja ikiwa ni miradi pamoja na ada mbalimbali,kichango,sadaka,mikopo
ubia na shughuli mbalimbali kutoka kwa wanachama.
b)
Matumizi ya fedha
(i)
Kununua mali ghafi kwa ajili ya kazi
za ushirika,
(ii)
Kuendesha matukio yote Muhimu ya
ushirika huu ikiwa ni pamoja na kusaidia katika shughuli za umoja ambazo ni
muhimu na zinahitaji fedha.
(iii)
Kusaidia wahitaji pale inapotokea
kwa makubalino ya wana uashika wa ngazi husika
(iv)
Safari za kikazi za viongozi,
watumishi au wawakilishi wa umoja kwenda kwenye matukio ya umoja na ya kijamii
yatakayohusisha ushirika huu.
(v)
Kutoa michango na kulipa kodi
mbalimbali
(vi)
SEHEMU YA NANE
Ibala 20:HAKI ZA USHIRIKA WA VIJANA
WA KIKRISTO TANZANIA
(i)
Ushirika wa vijana wa kikristo
tanzania utakuwa na haki ya kushitaki au kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za
nchi.
(ii)
Itakuwa na haki ya kubadili kifungu
chochote cha katiba hii kwa Msajili wa Vyama /Vikundi yaani BASATA lazima
ijulishwe mabadiliko ya katiba.
(iii)
utakuwa na haki ya kuhoji au
kuratibu/kusimamia shughuli yoyote ya vijana wa kikristo itakayo endeshwa
katika kila mkoa ikiwa na kwa vijana walio ndani ya umoja/ushirika huu.
SEHEMU YA TISA
Ibala 21: KUVUNJIKA/KUFA KWA
USHIRIKA.
Endapo
kikundi itavunjika mambo yafuatayo yatafanyika.
(i)
Itabidi kulipa madeni yote
yanayodaiwa kama yapo kwa wakati.
(ii)
Kudai mali au fedha zote zilizobaki kwa mtu
binafsi/ Taasisi iliyokubaliana naye kabla
(iii)
Kugawana mali yote iliyobaki kwa
usawa miongoni mwa Viongozi hai chini ya usimamini wa Viongozi wa Serikali Ya
Mtaa.
(iv)
Madeni yote yatalipwa na umoja huu
na yale ya kudai yatafuatiliwa na wadau wa umoja huu.
9.
MWISHO
Umoja
huu sio mali ya mtu binafsi au maslahi ya mtu au watu wachache isipo kuwa ni
kwaajili kristo na vijana wenye nia ya Kumtumikia Mungu.