Ijumaa, 28 Aprili 2017

UHALISIA WA MAISHA YA NDOA.
SEHEMU YA KWANZA
kabla hatuaja anagalia yaliyo katika ndoa Tutazame Maneno haya ya Daudi, Zaburi 127:1-2 "Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
Kwa wana ndoa na Wale wasio wana ndoa soma hii yaweza kusaidia
SEHEMU YA KWANZA.
UTANGULIZI:
Kwa kuanza tutazama haya maeneo kadhaa amabayo yanahusu ndoa nyingi za watu wenye maisha amabayo ni mfano mbele za watu lakini ndani ya ndoa yanaweza yakawa ni sehemu ya maisha yao na hawawezi mwambia mwingine au hata wakisema huwa hayana majibu na suluhu.
1. Wengi huwa na maswali kuhusu ndoa na wachache wanayo majibu ya maswali hayo. na wengine wanaishi katika ndoa lakini hawana majibu ya maswali ya yale yanayo endelea katika ndoa zao. hivyo huishi kwasababu kwa kuwa washafunga ndoa na hawana namna nyingine tena ya kubadili huo uhalisia.
2. Wengi huamini kuwa wamekosea au wamewahi kuoa na kuolewa na huyo mtu, na wengine ambao hawaja ingia katika ndoa hutazama watu vile wanaishi na kualinganisha na maisha wanayo tarajia katika ndoa na kuwafanya waogope kuingia katika ndoa au kuingia wakiwa na mashaka
3. Wengi husema mwenzi wake kabadilika mara baada ya kuingia katika ndoa na hajui kwanini. kabla ya kuingia katika ndoa alitamani awe na ndoa ya mfano, lakini kakutana na ndoa iliyo mjeruhi na kuendelea kumuumiza na kumfanya atake ndoa mpya "kitu kisicho wezekana"
4. Kabla ya kuingia kwenye ndoa mwenzi wako alikuwa anapendeza sana lakini baada ya kuolewa/kuoa hapendezi tena kama mwanzo, na hii imetambulika kwako na kwake imesabisha kupoteza uhuru wa kutoka faragha pamoja, au imekuwa sehemu ya wengine kuogopa kuoa na kuolewa.
5. Kabla ya kuingia kwenye ndoa mwenzi wako alikuwa anajari sana, anajitoa kwaajili yako, alikuwa anakushirikisha yote, alikuwa anakupa uhuru wote, alikuwa anakufanya mtu muhimu sana kwake lakini baada ya kuoa ua kuolewa mwenzi wako hana habari na wewe. hana muda wa kupanga na kujadili nawe. ndoto za wakati wa uchumba zimekufa, utekelezaji na utendaji wa mambo mema haupo tena, tabia usizo zijua ndoa zimetawala maisha yake.
NB: MASWALI YA KUJIULIZA:
i) KWANINI HAYA HUTOKEA
ii) JE MTU HUBADILIKA
III) kWANINI YATOKEE BAADA YA KUOA AU KUOLEWA
IV) JE NI KWELI UMEKOSEA KUOA AU KUOLEWA
V) JE NI KWELI MWENZI WAKO AKUPENDI
Tukutane sehemu ya Pili tuendelee kutazama ukweli katika ndoa!!
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Ndoa ni mwili moja: Ikiwa ni mwili mmoja unapaswa kuulisha, kuujali, na kuutunza kama vile unavyo fanya kwako mwenyewe, unapaswa kufanya zaidi kwa mwenzi wako.
By (THE VOICE OF VICTORY)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

UHALISIA WA MAISHA YA NDOA. SEHEMU YA KWANZA kabla hatuaja anagalia yaliyo katika ndoa Tutazame Maneno haya ya Daudi, Zaburi 127:1-2 &q...